Mfaham Tunda Man Hapa....

Baada ya kukutana na captain wa bongo flava Tanzania Tunda man nilipiganae story kuhusu maisha yake ya kimuziki pamoja na maisha ya kawaida, na haya ndiyo yalikua mazungumzo yetu.
Tunda
HZB: Inakuaje captain?   Tunda: Baridi mwana. HZB: hebu niambie majina yako kamili. Tunda: me naitwa Khaleed Ramadhan Tunda. HZB: Vp kuhusu kiwango chako cha elimu? Tunda: Mimi nimesoma mpaka form four na shule ya msingi nilisoma pale Mwl Nyerere primary school,na sekondari ilikua  Forodhan secondary school. HZB:Wakati unakua ulifikiria kama utakuja kufanya muziki? Tunda:hapana nilikua napenda sana niwe doctor, lakini nilijikuta nacheza mpira (Kipa) na badae nikawa naandika sana mistari na nimewaandikia wengi tu lakini nikajikuta na mimi naweza kuimba ndipo nikaingia rasmi kwenye game.
HZB: Mwanzo ulikua katika kundi la lafamilia ambalo lilikua likiongozwa na chid benz na kwa sasa wewe ndo msimamizi wa kazi za chidi benzi ikoje hiyo? Tunda; yaah nikweli chid benz n brother wangu na anajua sana yaan ni bonge la rapper laikini kwa sasa naona kama kakata tamaa ya kufanya muziki, nikaona nisimamie kazizake kwasababu namkubali sana chidi.
Chid
HZB: Mpaka sasa una albamu ngapi?na je kwa gemu ya sasa ilivyo unafikiria kutoa albamu nyingine?  Tunda:nina albamu tatu Naila,Nipe riport pamoja na Hali yangu mbaya, na kwa sasa natarajia kutoa albamu ya nne ambayo itaitwa Wanaona haya ikiwa na jumla ya nyimbo 18. HZB: Ni msanii gani alieye kushawishi kufanya muziki kutokana na uimbaji wake? Tunda: daah Ferooz wa daz nundazi.
Ferooz
HZB:Ni producer gani unamkubali bongo? Tunda: manecky
Tunda & Maneck
HZB:Ni ngoma gani ambayo umefanya na unaikubali sana? Tunda: demu siyo coz ni ngoma ambayo ni yatofauti sana na muziki ambao naufanya. HZB: Ni msanii gani unatamani kufanyanae kazi East Africa? Tunda: Jose Chamillion, namkubali sana pia jinsi ambavyo anaimba so nikifanyanae nahisi tutafanya kiyu kizuri. HZB:kutoka Khaleed mpaka sasa Tunda man ni ugumu gani ulioupata? Tunda:daah tumepata shida sana kurekod pia nimetembea sana kwa mguu kwenda studio na ukifika unazinguliwa kinoma.
Tunda on the mic
HZB:Tofauti na muziki ni kitu gani kingine unafanya? Tunda: Tofauti na muziki mimi nafanya biashara tu ndogondogo. HZB: Mwaka ndo kama unaisha hivi,je mashabiki wako wategemee nini kwa mwaka ujao 2013? Tunda:watarajie vitu vingi tu kama hiyo albamu ya nne pia video yangu mpya ya wanaona haya wimbo ambao nimefanya na chege,Tayari nimeshaongea na Ogopa deejs na kila kitu fresh siku yeyote ntaondoka kuelekea Nairobi. HZB:Kuna wimbo ambao umefanya wewe pamoja na marehemu sharo,lakini wewe kama ukazingua siku ya video haukutokea je unampango wowote kuhusu ngoma hiyo? Tunda:Yaah mpango upo nitaifanya ile video kama kumuenzi marehem sharo,na sikufanya makusudi siku hiyo nilipata dharura nikawa nimeenda Arusha kikazi nikawa nimeshindwa kufanya video hiyo. HZB: Turudi kwa maisha ya kawaida, je umeoa? na unawatoto wangapi? Tunda: mimi sijaoa bado ila nina mtoto mmoja wa kike anaitwa Khayraty,nampenda sana.
Khayraty
HZB:Unatoa ushauri gani kwa wasanii ambao wanaanza na wanataka kufika ulipofika wewe? Tunda:heshima tu kwa sababu bila heshima hawawezi kufanikiwa,pia wengine wanakuja mikono nyuma na wakisaidiwa tu wakasikika kidogo wanaanza dharau,hiyo mbaya sana. HZB:Neno lolote la mwisho kwa mashabiki wako? Tunda:mashabiki wangu nawapenda sana pia wakae tayari kwa ngoma yangu mpya wanaona haya pamoja na albamu ya nne yenye jumla ya nyimbo 18, Pia wategemee show kali sana kila nitakapopanda jukwaani na wana ndumi.
Tunda & Wana ndumi

0 comments:

Copyright © 2014 TipTop Connection and Blogger Templates - John Sambila.