Showing posts with label tiptopconnection blog. Show all posts

BABU TALE AELEZEA CHANZO CHA KIFO CHA KAKA YAKE ABDU BONGE



Abdu Bonge aliekuwa Meneja aliekuwa akiongoza Kundi la Muziki la Tiptop Connection akisaidia na Mdogo wake Babu Tale alifariki Dunia jana Jioni, Taarifa za Mwanzo hazikuweza kueleza kuhusu chanzo cha kifo chake lakini leo Mdogo wake Babu Tale ameelezea Jinsi ambavyo kaka yake alipoteza Maisha.
‘Kuna mshkaji wetu mmoja alikua anagombana na mke wake jirani yetu, wakamfata hapa Abdul aende… mara ya kwanza na ya pili akakataa, mara ya tatu akasema ngoja aende’
‘Alivyoenda ukapita ukimya kidogo, baadae kuna mtu akaja kumuita kaka yetu mkubwa mwingine na kumwambia nenda kamsaidie kaka yako mkubwa amedondoka, kaka yangu baadae akanipigia simu akasema Bonge kama amezimia lakini sidhani kama atapona sababu wakati wa kuamulia ugomvi alianguka baada ya kusukumwa nafikiria aliangukia kichogo, kumpeleka Hospitali Manzese wakasema ameshafariki‘ alisema  Babu Tale.

PICHA; MSIBANI TIPTOP CONNECTION


Abdu Bonge alifariki jana Nyumbani majira ya Jioni alipokuwa akiamulia ogovi wa watu wake wa karibu ndipo alianguka vibaya kwenye sakafu na kupoteza Maisha, Mwili bado uko hosptal kwa Uchunguzi zaidi na taratibu zikikamilika kesho mwili utasafirishwa kuelekea Morogoro Mbuyuni Kilometa takribani 100 kutokea Morogoro Mjini ambako ni Nyumbani kwa Marehemu. kwa sasa msiba upo Magomeni Njiapanda ya Kagera maskani ya Tiptop Connection.

PICHA ZAIDI INGIA >>HARAKATI ZA BONGO
 MB Doggy Msanii kutoka TipTop Connection akizungumza jambo na Rafiki waliotembelea Msibani hapo.
 Mkubwa Fella akipitisha Daftari la michango kwa Ndugu na Jamaa waliofika Msibani.
 Mdogo wa Marehemu Mjomba Iddi mwenye Fulana Nyekundu akizungumza jambo na Rafiki Msibani hapo.
 Mdogo wa Marehemu Kwembe Taletale a.k.a DJ K Man mwenye Fulana Nyeusi akizungumza jambo na Ndugu na Jamaa Msibani hapo.
 Tunda man Akilia kwa Uchungu kabisa akiwa na Babu Tale Msibani Magomeni Njiapanda ya Kagera Maskani ya Tiptop Connection.

BIG UP DIAMOND PLATNUMZ

Asie kubali kushindwa si Mshindani ni Msemo ambo umezoeleka sana na pengine masikio yako yameisha sikia sana hiki kitu lakini ndiyo ukweli ulivyo, Kufika tu huko na kuchaguliwa kuwania Tuzo za BET ni Hatua kubwa sana katika Muziki wetu, kwani ni mara ya kwanza msanii kutoka Tanzania na kwenda kushiriki katika Tuzo kubwa Duniani za BET. Tunakupongeza sana Bwana Diamond Platnumz Japo Ushindi haujaja nyumbani lakini tunaamini Wakati ujao basi tunaweza na sisi Tukaishangaza Dunia.

Unatuonyesha njia na kututia hamasa ya Kufanya Kazi nzuri na kujituma zaidi kila jua lichomozapo ili tufike Mbali zaidi, Eeeh mwenyezi Mungu Tusaidie

Sikiliza na Download Track Mpya Ya Madee ~ Tema Mate Tuwachape [Audio]


Meneja wa Kundi la TipTop Connection, Babu Tale Apata Mtoto wa Kiume

 Manager wa Kundi la Tiptop Connection Hamis Shabani Taletale Maarufu kwa jina la Babu Tale amebahatika kupata Mtoto Mwingine wa Kiume usiku wa Kuamkia Leo katika Hosptal ya Taifa Muhimbili ambako Mke wake alijifungua.
Babu Tale alishukuru Mungu kwa Mke wake kujifungua Salama na Kuweza kumletea Mtoto Mwingine wa Kike ambapo Mtoto wa Kwanza walimpata Miaka sita iliyopita.
Hongera sana Babu Tale pamoja na Mama Tale
Picha Hii Ni Mtoto Mgeni na pembeni ni Bab Tale pamoja na Mkewe na Mtoto wao Tale

Fiesta 2013 ndani ya Jiji la Mbeya ni Noma sana...

Afande Sele kwa Stage
Mkali Aliyetokea BSS Wolter Chilambo
Tajiri wa Mahaba Kassim Mgaga
Madee On Stage
Mavoko
Temba na Chege
Nay Wa Mitego
Naylee
Shilole
Stamina
Young Killer
Zillah

Take it from me, wengine feki tu.... today @ Serena Hotel | From 20:00 to 21:00 #NumberOne…

Take it from me, wengine feki tu.... today @ Serena Hotel | From 20:00 to 21:00 #NumberOne…

Track; Asali ~ Mzuri "Sikiliza na Download"

Track; Mirror ~ Baby "Sikiliza na Download"

TRACK: Dogo Aslay Ft Linah ~ Bado Mdogo

TRACK: Raymond ~ Jikatae "Sikiliza na Download"

Video: E-Joh ft Tunda Man ~ Sichezi na wewe

NYUMA YA PAZIA: CASTOR AKIPIGA STORY NA CAPTAIN WA BONGO FLEVA "TUNDA MAN" KATIKA KIBALAZA CHA GETTO LA MWANANCHI WA KAWAIDA SIZ KITAA

Custor akimpokea tunda akiwa na Team yake Fadhili pamoja na zungu
Baada ya kufika katika kibalaza cha getto la mwananchi na story kuanza
Hapa Captain akikumbuka story katika zile story tatu
HApa  akielezea safari yake ya kimuziki na kuhama La Familia mpka Tiptop Connection
Copyright © 2014 TipTop Connection and Blogger Templates - John Sambila.