Showing posts with label tunda man. Show all posts

Picha:Yaliyojiri kwenye uzinduzi wa simu mpya 'Nokia X' jijini Dar es Salaam, TipTop Connection Walikiwasha

Usiku wa kuamkia leo Nokia yazindua simu mpya 'NOKIA X' itakayokuwa na matumizi yote kwa wateja wake (Adroid) yenye uwezo wa kuwa na mitandao ya kijamii ikiwemo
Facebook,Skype,Vibe,Instagram,Twitter,uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Samaki Samaki uliopo Posta jijini Dar es Salaam.
Kwenye Uzinduzi huo pia wageni waalikwa na wadau mbalimbali walipata burudani kali kutoka kwa wasanii wa Tip Top Connection Tunda Man na Madee.

Tunda Man Kuzindua Video ya Msambinungwa Leo Jumapili Ndani ya Club 71 Tegeta


Ni jumapili hii pale club 71 Tegeta moto utawashwa na Captain wa Bongo Fleve @tundamanofficial na @alikiba4real .....ni katika uzinduzi wa chupa la #msambinungwa pia team nzima ya @tiptopconnection itakuwepo na watakiwasha...sasa kwanini ukose ..njoo uone show kali ya @tundamanofficial akifanya tofauti na zile zote ulizowahi kuziona , @madeeali @babutale @mkubwafella

New Video: Tunda Man Ft Ally Kiba ~ Msambinugwa


Tunda Man Kuachia Video ya Msambinugwa na Album ya Qaswida Hivi Karibuni

Captain wa Bongo Flea Anatarajia kuachia Video yake Mpya Hivi Karibuni, Ambayo ameshoot hapa Bongo na Nyingine Amefanyia Kenya, Katika Video Hiyo utamuona Masogage pamoja na Ally Kiba..
Video iko kamili na Wiki Hii Itaachiwa.
Ally Kiba
Kwa Upande Mwingine Amesema Anatarajia Kuachia Album yake ya Kaswida, Ambapo alisema kuwa licha ya Kufanya Mziki wa Bongo Fleva lakini yeye ni Mtoto wa Kiislam anaitwa Khalid hivyo Anapaswa kumkubuka Mungu, Album iko Tayari nBado Wimbo Mmoja pia Katika Album Hiyo Utwasaikia wasanii Kama Kassim Mgaga pamoja na Daina, Tunda alisema Daina ni Mkristo lakini alimuelekeza jinsi ya Kupita katika Njia za Kiislamu na Kafanya Vizuri.
Daina Nyange
Cassim Mganga
Ugum Mwingine alioupata ni Stuo kwa Manecky Alisema Kuwa Manecky ni Emmanuel yaani Mkristo Ivyo Hajawahi kupiga Dufu hata Siku Moja so ili Bidi nimuelekeze lakini kafanya Vizuri.
Maneck
Naamini album Nii Kali sana Pia sito peleka kwa Muindi Nitaisambaza Mikoani na Nyingine Ntauza Mwenyewe Mkononi, Alisema Tunda Man.

Unamkumbuka Huyu Mzungu aliyekuwaga BSS Alipoimba wimbo wa Nipe Riport


yakale n Dhahabu hivyo sio Mbaya kukumbuka huyu jamaa n Mzungu na alikuwa Mshiriki wa Mashindano ya BSS ambayo hufanyika kila mwaka hapa Nchini... Kitu ambacho kimenifanya kulikumbuka hili Ni pale alipoimba wimbo wa Nipe riport akiwa na Tunda Man katika Fainal za Mashindano hayo Ilikua poa sana Kwakweli

wewe unakumbuka Tukio Gani kuhusu huyu Mzungu..

Nyuma ya Camera, Tunda Man katika Movie Mpya ya TipTop Connection "Ndoa"

 Ndoa Ndiyo Movie mpya kutoka TipTop Connection ambayo inafuta baada ya zile zote ambazo umeziona
Humu ndani kuna wakali Kibao katika Movie pamoja na Captain wa Bongo Fleva Tunda Man.
Jipange kwa Mzigo huu nakuahidi n Noma sanaaa


Msambinungwa - Tundaman Ft. Alikiba [Audio]


Sikiliza Track Hii Kutoka Tiptop Sungura na Tunda Man ~ Naipenda TipTop [Audio]

Bongo Fleva Newz; Tunda Man: Akanusha Taarifa zilizo tolewa kuwa kakimbia Poli nusu uchi kisa Deni, Alichokisema kiko hapa....

Mkali kutoka TipTop Connection Captain wa Bongo Fleva Tunda Man, Amekanusha Taarifa zilizo tolewa na Blog moja hapa Mjini Kuhusu yeye kukimbia kwa Deni la Laki Nane akiwa Nusu Uchi. Baada ya Polisi kufika nyumbani kwake,kumkamata kwa kutolipa deni hilo etii alilokopa kwa mdada ambbaye jina lake halikutajwa. Tunda man amesema kuwa" Nawaomba sana hao watu wa Blog waandike Habari zenye uhakika yaani wasikilize pande zote mbili sio kumsikiliza mtu mmoja tu kisha wana andika habari, kwanini asinipigie simu baada ya kusikia taarifa hizo ili mimi nimuhakikishie? watu wengine wanapenda kualibiana majina tu, Mimi show Moja nalipwa Hela nyingi tu siwezi kukimbia Deni Hilo huko ni kuchafuana tu" Alisema tunda man....

Video: E-Joh ft Tunda Man ~ Sichezi na wewe

Video: D Boy Ft Tunda man & Sungura ~ Mapenzi Hayalazimishwi

Mfaham Tunda Man Hapa....

Baada ya kukutana na captain wa bongo flava Tanzania Tunda man nilipiganae story kuhusu maisha yake ya kimuziki pamoja na maisha ya kawaida, na haya ndiyo yalikua mazungumzo yetu.
Tunda
HZB: Inakuaje captain?   Tunda: Baridi mwana. HZB: hebu niambie majina yako kamili. Tunda: me naitwa Khaleed Ramadhan Tunda. HZB: Vp kuhusu kiwango chako cha elimu? Tunda: Mimi nimesoma mpaka form four na shule ya msingi nilisoma pale Mwl Nyerere primary school,na sekondari ilikua  Forodhan secondary school. HZB:Wakati unakua ulifikiria kama utakuja kufanya muziki? Tunda:hapana nilikua napenda sana niwe doctor, lakini nilijikuta nacheza mpira (Kipa) na badae nikawa naandika sana mistari na nimewaandikia wengi tu lakini nikajikuta na mimi naweza kuimba ndipo nikaingia rasmi kwenye game.
HZB: Mwanzo ulikua katika kundi la lafamilia ambalo lilikua likiongozwa na chid benz na kwa sasa wewe ndo msimamizi wa kazi za chidi benzi ikoje hiyo? Tunda; yaah nikweli chid benz n brother wangu na anajua sana yaan ni bonge la rapper laikini kwa sasa naona kama kakata tamaa ya kufanya muziki, nikaona nisimamie kazizake kwasababu namkubali sana chidi.
Chid
HZB: Mpaka sasa una albamu ngapi?na je kwa gemu ya sasa ilivyo unafikiria kutoa albamu nyingine?  Tunda:nina albamu tatu Naila,Nipe riport pamoja na Hali yangu mbaya, na kwa sasa natarajia kutoa albamu ya nne ambayo itaitwa Wanaona haya ikiwa na jumla ya nyimbo 18. HZB: Ni msanii gani alieye kushawishi kufanya muziki kutokana na uimbaji wake? Tunda: daah Ferooz wa daz nundazi.
Ferooz
HZB:Ni producer gani unamkubali bongo? Tunda: manecky
Tunda & Maneck
HZB:Ni ngoma gani ambayo umefanya na unaikubali sana? Tunda: demu siyo coz ni ngoma ambayo ni yatofauti sana na muziki ambao naufanya. HZB: Ni msanii gani unatamani kufanyanae kazi East Africa? Tunda: Jose Chamillion, namkubali sana pia jinsi ambavyo anaimba so nikifanyanae nahisi tutafanya kiyu kizuri. HZB:kutoka Khaleed mpaka sasa Tunda man ni ugumu gani ulioupata? Tunda:daah tumepata shida sana kurekod pia nimetembea sana kwa mguu kwenda studio na ukifika unazinguliwa kinoma.
Tunda on the mic
HZB:Tofauti na muziki ni kitu gani kingine unafanya? Tunda: Tofauti na muziki mimi nafanya biashara tu ndogondogo. HZB: Mwaka ndo kama unaisha hivi,je mashabiki wako wategemee nini kwa mwaka ujao 2013? Tunda:watarajie vitu vingi tu kama hiyo albamu ya nne pia video yangu mpya ya wanaona haya wimbo ambao nimefanya na chege,Tayari nimeshaongea na Ogopa deejs na kila kitu fresh siku yeyote ntaondoka kuelekea Nairobi. HZB:Kuna wimbo ambao umefanya wewe pamoja na marehemu sharo,lakini wewe kama ukazingua siku ya video haukutokea je unampango wowote kuhusu ngoma hiyo? Tunda:Yaah mpango upo nitaifanya ile video kama kumuenzi marehem sharo,na sikufanya makusudi siku hiyo nilipata dharura nikawa nimeenda Arusha kikazi nikawa nimeshindwa kufanya video hiyo. HZB: Turudi kwa maisha ya kawaida, je umeoa? na unawatoto wangapi? Tunda: mimi sijaoa bado ila nina mtoto mmoja wa kike anaitwa Khayraty,nampenda sana.
Khayraty
HZB:Unatoa ushauri gani kwa wasanii ambao wanaanza na wanataka kufika ulipofika wewe? Tunda:heshima tu kwa sababu bila heshima hawawezi kufanikiwa,pia wengine wanakuja mikono nyuma na wakisaidiwa tu wakasikika kidogo wanaanza dharau,hiyo mbaya sana. HZB:Neno lolote la mwisho kwa mashabiki wako? Tunda:mashabiki wangu nawapenda sana pia wakae tayari kwa ngoma yangu mpya wanaona haya pamoja na albamu ya nne yenye jumla ya nyimbo 18, Pia wategemee show kali sana kila nitakapopanda jukwaani na wana ndumi.
Tunda & Wana ndumi

Video; JUMA NATURE FT TUNDA MAN ~ HAIPOTEI

NYUMA YA PAZIA: CASTOR AKIPIGA STORY NA CAPTAIN WA BONGO FLEVA "TUNDA MAN" KATIKA KIBALAZA CHA GETTO LA MWANANCHI WA KAWAIDA SIZ KITAA

Custor akimpokea tunda akiwa na Team yake Fadhili pamoja na zungu
Baada ya kufika katika kibalaza cha getto la mwananchi na story kuanza
Hapa Captain akikumbuka story katika zile story tatu
HApa  akielezea safari yake ya kimuziki na kuhama La Familia mpka Tiptop Connection

Picha 3 za Tundaman Mbele ya Camera akishoot Movie mpya kutoka Tiptop Connection "NDOA"

Baada ya Movie ya Nipe Riport kufanya poa katika Hood sasa TipTop Connection wanapika Movi jingine "Ndoa" soon itaingia mtaani Angalia hizi picha tatu Tundaman akicheza semu yake.......

Kama ulikuwa Bado Haujasikia Qaswida ya Tunda Man Iko Hapa

Msanii wa Bongo Fleva Tanzania Khalid Ramadhani Tunda, Maarufu kama Tunda Man Ameandaa album ya Qaswida imbayo inaitwa TUFUNGENI NA KUSWALI. Ambayo imebeba Jumla ya Nyimbo 6.
Tunda man Captain wa Bongo Fleva Tanzania Ameamua kuwakumbusha waislamu wote KUFUNGA NA KUSWALI Katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Unaweza kusikiliza wimbo ambao umebeba jina la Album hiyo.....
Copyright © 2014 TipTop Connection and Blogger Templates - John Sambila.