Mkubwa Fella ampatia Nyumba yenye Thamani ya Milioni 20 Mh. Temba

 Meneja wa Kundi la Muziki la TMK Wanaume Familly lenye Maskani yake Temeke, Saidi Mlinge maarufu kwa Jina la Mkubwa Fella Amemkabidhi Nyumba Moja ya Msanii wa Kundi hilo, Mh. Temba. Fella amempatia nyumba nzima Temba ikiwa imekamilika pia amesema amesha fanya hivyo kwa sanii wengi aliokuwa anawasimamia ambao wengine hataki kutajwa kama walishawahi kupatiwa nyumba. Kwa upande wangu nachukua nafasi hii kumpongeza Fella kwa kitu alichokifanya Maana wasanii wengi hujisahau pindi wanapokuwa Juu, Muda mwingi wanaupoteza katika starehe wala hafikirii kuwa iko siku muziki wake utashuka na kukosa hata pakujistili ndipo stress zinaanza na hata kuanza kufanya mambo ya ajabu katika Jamii.

0 comments:

Copyright © 2014 TipTop Connection and Blogger Templates - John Sambila.