Showing posts with label habari. Show all posts

BABU TALE AELEZEA CHANZO CHA KIFO CHA KAKA YAKE ABDU BONGE



Abdu Bonge aliekuwa Meneja aliekuwa akiongoza Kundi la Muziki la Tiptop Connection akisaidia na Mdogo wake Babu Tale alifariki Dunia jana Jioni, Taarifa za Mwanzo hazikuweza kueleza kuhusu chanzo cha kifo chake lakini leo Mdogo wake Babu Tale ameelezea Jinsi ambavyo kaka yake alipoteza Maisha.
‘Kuna mshkaji wetu mmoja alikua anagombana na mke wake jirani yetu, wakamfata hapa Abdul aende… mara ya kwanza na ya pili akakataa, mara ya tatu akasema ngoja aende’
‘Alivyoenda ukapita ukimya kidogo, baadae kuna mtu akaja kumuita kaka yetu mkubwa mwingine na kumwambia nenda kamsaidie kaka yako mkubwa amedondoka, kaka yangu baadae akanipigia simu akasema Bonge kama amezimia lakini sidhani kama atapona sababu wakati wa kuamulia ugomvi alianguka baada ya kusukumwa nafikiria aliangukia kichogo, kumpeleka Hospitali Manzese wakasema ameshafariki‘ alisema  Babu Tale.

PICHA; MSIBANI TIPTOP CONNECTION


Abdu Bonge alifariki jana Nyumbani majira ya Jioni alipokuwa akiamulia ogovi wa watu wake wa karibu ndipo alianguka vibaya kwenye sakafu na kupoteza Maisha, Mwili bado uko hosptal kwa Uchunguzi zaidi na taratibu zikikamilika kesho mwili utasafirishwa kuelekea Morogoro Mbuyuni Kilometa takribani 100 kutokea Morogoro Mjini ambako ni Nyumbani kwa Marehemu. kwa sasa msiba upo Magomeni Njiapanda ya Kagera maskani ya Tiptop Connection.

PICHA ZAIDI INGIA >>HARAKATI ZA BONGO
 MB Doggy Msanii kutoka TipTop Connection akizungumza jambo na Rafiki waliotembelea Msibani hapo.
 Mkubwa Fella akipitisha Daftari la michango kwa Ndugu na Jamaa waliofika Msibani.
 Mdogo wa Marehemu Mjomba Iddi mwenye Fulana Nyekundu akizungumza jambo na Rafiki Msibani hapo.
 Mdogo wa Marehemu Kwembe Taletale a.k.a DJ K Man mwenye Fulana Nyeusi akizungumza jambo na Ndugu na Jamaa Msibani hapo.
 Tunda man Akilia kwa Uchungu kabisa akiwa na Babu Tale Msibani Magomeni Njiapanda ya Kagera Maskani ya Tiptop Connection.

BIG UP DIAMOND PLATNUMZ

Asie kubali kushindwa si Mshindani ni Msemo ambo umezoeleka sana na pengine masikio yako yameisha sikia sana hiki kitu lakini ndiyo ukweli ulivyo, Kufika tu huko na kuchaguliwa kuwania Tuzo za BET ni Hatua kubwa sana katika Muziki wetu, kwani ni mara ya kwanza msanii kutoka Tanzania na kwenda kushiriki katika Tuzo kubwa Duniani za BET. Tunakupongeza sana Bwana Diamond Platnumz Japo Ushindi haujaja nyumbani lakini tunaamini Wakati ujao basi tunaweza na sisi Tukaishangaza Dunia.

Unatuonyesha njia na kututia hamasa ya Kufanya Kazi nzuri na kujituma zaidi kila jua lichomozapo ili tufike Mbali zaidi, Eeeh mwenyezi Mungu Tusaidie

Kauli ya babu Tale na Madee Kuhusu Dogo Janja Kuomba Msamaha

Dogo Janja kuuomba msamaha kupitia vyombo vya habari uongozi wa Tip Top Connection na Madee aliyemtoa Arusha, Boss wa Tip Top Connection Babu Tale Amezungumza kuwa  anataka rapper huyo aseme ukweli wa yote aliyoyasema awali baada ya kutoka Tip Top.
“Aongee ukweli tu haina shida, nimemsamehe yeye ni Muislamu mwenzangu tumetumwa tusameheane, mimi nimeshamsamehe ila nimezungukwa na mashabiki ambao wakati yeye ananitukana kuna mashabiki ambao walikuwa upande wangu ingawa walikuwa hawajui kama dogo alikuwa anaongea ukweli au uongo.” Amesema Babu Tale.
“Babu Tale ameweka wazi vipengele ambavyo anataka Dogo Janja aviweke sawa.
“Dogo anatakiwa aseme kama kweli aliibiwa, kama kweli alidhurumiwa na kama kweli hajawahi kuishi nyumbani kwa Madee. Anatakiwa aongee dhahiri asifiche, aongee tu ukweli.” Babu Tale ameeleza.
Amegusia pia tukio ambalo lilimsikitisha zaidi wakati Dogo Janja anafanya kazi akiwa chini ya menejimenti ya Mtanashati Entertainment.
“Siku zote kwenye ukweli uongo hujitenga, wakati yuko South Africa alipost picha ‘ningekuwa Tip Top nisingefika huku’. Nilishangaa heeh huyu kutoka huko kijijini kwao alifanyaje hadi kufika hapa!
“Wazazi wake nao wakawa wamekubali uongo wa mtoto wao wakaanza kutuongelea na sisi maneno ambayo ni uongo. Ulikuwa uongo wa watoto halafu bado wao wanakandamiza uongo zaidi ya uongo. Kwa kuwa ni mtoto kuna wazazi ambao walisimama nyuma yake ambao nao walikuwa wanasapoti. Aongee ukweli mimi ntamsaidia.” Babu Tale ameeleza.
Babu Tale ameeleza kuwa Dogo Janja ameshamtafuta kwa njia ya simu lakini amemwambia ujumbe ule ule kuwa awaambie ukweli watanzania.
Kwa upande wa dogo janja, ameongea na hakutaka kuizungumzia kwa undani kauli ya Babu Tale, zaidi alieleza kuwa alichokifanya kuomba msamaha alimaanisha kuwa alikuwa amekosea na hakuna aliyemsukuma kufanya hivyo.
Ameeleza kuwa endapo atakaribishwa tena Tip Top Connection atajiunga na kundi hilo japo ameeleza kuwa kuomba kwake msamaha hakuwa na maana kuwa alikuwa na lengo la kurudi Tip Top.
“Mimi nimeomba msamaha kwa kuwa nataka kuweka mambo sawa na kumaliza tofauti na uongozi wangu wa zamani. Hivyo tu. Wakinikaribisha Tip Top itakuwa poa tu pia…fresh.”
Kwa upande wa Madee ambaye alisema kuwa bado hajawa tayari kuongelea suala hilo na kwamba mtu anaeweza kuzungumzia suala hilo kwa sasa ni Babu Tale.

Ditto Kuachia "Tuongeze Bidii" Baada ya Kimya Cha Muda

Mkali kutoka THT Ditto kesho anataraji kuachia kazi yake Mpya Tuongeze Bidii baada ya Kuwa kimya Kwa Muda Kidogo.
Kama ulimmiss kwenye Game Ditto basi Kesho fanya kupitia Hapa Ili kuisikiliza Kazi yake hiyo Mpya.

Jinsi Tapeli alivyotaka Kumtapeli Madee

Akili Mjini Nguvu Shamba...Tapali ayakanyaga kwa Mtoto wa Manzese Madee Jamaa huyu alitaka kumtapeli Madee kwa Kusema Ati Geez Mabovu anaumwa Figo na Yeye ndo Mkusanyaji wa Mchango kwa Ajili ya Matibabu ya Ugonjwa Huo...
Alikua akipiga simu nyingi tu kwa Madee na kusisitiza Kuwa amtumie pesa hiyo kwa Ajili ya Mchango, Madee akafanya kumvuta Maskani ya Tiptop aje kuchukua pesa hiyo na Baada ya kufika Ndipo akahojiwa Maswali na kugundulika kuwa ni Tapeli na sio ndugu wala Jamaa wa Geez Mabovu.

Mkubwa Fella ampatia Nyumba yenye Thamani ya Milioni 20 Mh. Temba

 Meneja wa Kundi la Muziki la TMK Wanaume Familly lenye Maskani yake Temeke, Saidi Mlinge maarufu kwa Jina la Mkubwa Fella Amemkabidhi Nyumba Moja ya Msanii wa Kundi hilo, Mh. Temba. Fella amempatia nyumba nzima Temba ikiwa imekamilika pia amesema amesha fanya hivyo kwa sanii wengi aliokuwa anawasimamia ambao wengine hataki kutajwa kama walishawahi kupatiwa nyumba. Kwa upande wangu nachukua nafasi hii kumpongeza Fella kwa kitu alichokifanya Maana wasanii wengi hujisahau pindi wanapokuwa Juu, Muda mwingi wanaupoteza katika starehe wala hafikirii kuwa iko siku muziki wake utashuka na kukosa hata pakujistili ndipo stress zinaanza na hata kuanza kufanya mambo ya ajabu katika Jamii.

Tunda Man Kuzindua Video ya Msambinungwa Leo Jumapili Ndani ya Club 71 Tegeta


Ni jumapili hii pale club 71 Tegeta moto utawashwa na Captain wa Bongo Fleve @tundamanofficial na @alikiba4real .....ni katika uzinduzi wa chupa la #msambinungwa pia team nzima ya @tiptopconnection itakuwepo na watakiwasha...sasa kwanini ukose ..njoo uone show kali ya @tundamanofficial akifanya tofauti na zile zote ulizowahi kuziona , @madeeali @babutale @mkubwafella

Tunda Man Kuachia Video ya Msambinugwa na Album ya Qaswida Hivi Karibuni

Captain wa Bongo Flea Anatarajia kuachia Video yake Mpya Hivi Karibuni, Ambayo ameshoot hapa Bongo na Nyingine Amefanyia Kenya, Katika Video Hiyo utamuona Masogage pamoja na Ally Kiba..
Video iko kamili na Wiki Hii Itaachiwa.
Ally Kiba
Kwa Upande Mwingine Amesema Anatarajia Kuachia Album yake ya Kaswida, Ambapo alisema kuwa licha ya Kufanya Mziki wa Bongo Fleva lakini yeye ni Mtoto wa Kiislam anaitwa Khalid hivyo Anapaswa kumkubuka Mungu, Album iko Tayari nBado Wimbo Mmoja pia Katika Album Hiyo Utwasaikia wasanii Kama Kassim Mgaga pamoja na Daina, Tunda alisema Daina ni Mkristo lakini alimuelekeza jinsi ya Kupita katika Njia za Kiislamu na Kafanya Vizuri.
Daina Nyange
Cassim Mganga
Ugum Mwingine alioupata ni Stuo kwa Manecky Alisema Kuwa Manecky ni Emmanuel yaani Mkristo Ivyo Hajawahi kupiga Dufu hata Siku Moja so ili Bidi nimuelekeze lakini kafanya Vizuri.
Maneck
Naamini album Nii Kali sana Pia sito peleka kwa Muindi Nitaisambaza Mikoani na Nyingine Ntauza Mwenyewe Mkononi, Alisema Tunda Man.

Chege na Temba Wajipanga Kuja kivingine Safari hiii


Baada ya Ukimya wa Muda Mrefu kidogo sasa Chege na Temba wako studio wakiandaa Kazi yao Mpya Chini ya Producer Shiricom katika Studio za Mkubwa na Wanawe.. 

Kwa sasa wameamua kufanya Mziki wa Biashara na hata Ngoma hiyo inayofanyika ukiisikia lazima utaielewa tu ni bonge moja ya Ngoma Mdundo pia Ni hatarii. 

Track hiyo inatarajiwa Kutoka Mapema Mwezi wa Tatu,Kama Ulimiss Kitu kutoka Kwa Hawa Jamaa Jipange kuwapokea na Ujio wao Huu Mpya.

Mkubwa na wanawe Centre wafungua studio Nyingine Mkoani Mtwara

 Mkubwa na wanawe music center imefungua studio nyingine mkoani Mtwara, ikiwa na lengo la kuinua vipaji vya muziki hata vilivyojificha.
 Studio inaitwa MKUBWA MUSIC na producer ni  Zest Mkali karibun wadau wote wa muziki tanzania

Jipange Kusikia Pombe yangu RMX kutoka kwa Madee na P-Unit


Baada ya kufanya vizuri na kuwa Gumzo kila kona ya Bongo yaani Wimbo wataifa "Pombe yangu" kutoka kwa Rais wa Manzese Madee, Sasa tarajia RMX ya ngoma hii hivi katibuni na wababe wengine wa muziki kutoka Kenya P-Unit. 
 Mzigo umefanyika kwa Marco Chali kama kwa na Wiki ijayo Madee ataenda Kenya kwa ajili ya Video na Kisha mzigo unaachiwa
Usikose kutembelea Hapa. ili uwe wa kwanza kusikiliza na Kudownload

Video ya Tema Mate Kuachiwa Kesho...

Video ya wimbo wa Tema mate..
 kesho inatoka Rasmi
 mzigo umefanywa na ma Director wazoefu kabisa na wanao kimbiza kwenye utengenezaji wa Video kwa sasa
 Ogopa Djz 
Usikose kutembelea hapa kesho Mapema ili Kuangalia Video Hiyoo
Much Lov kwa Fans Wote wa Tiptop Connection na Madee

Meneja wa Kundi la TipTop Connection, Babu Tale Apata Mtoto wa Kiume

 Manager wa Kundi la Tiptop Connection Hamis Shabani Taletale Maarufu kwa jina la Babu Tale amebahatika kupata Mtoto Mwingine wa Kiume usiku wa Kuamkia Leo katika Hosptal ya Taifa Muhimbili ambako Mke wake alijifungua.
Babu Tale alishukuru Mungu kwa Mke wake kujifungua Salama na Kuweza kumletea Mtoto Mwingine wa Kike ambapo Mtoto wa Kwanza walimpata Miaka sita iliyopita.
Hongera sana Babu Tale pamoja na Mama Tale
Picha Hii Ni Mtoto Mgeni na pembeni ni Bab Tale pamoja na Mkewe na Mtoto wao Tale

Coming Soon: Baada ya Pombe yangu sasa Madee na ujio wa Tema Mate Tuwachape.

Kutoka Tiptop Connection, Madee kwa sasa anakuja na Track ya Tema mate tuwachape, ambayo imefanyika ndani ya Studio za MJ na Producer Marco Chali..

Unajua Madee kafanya nini kwa sasa katika Track Hii, andaa sikio lako kisha endelea kutembelea hapa Siku si nyingi utakutana na kazi hii.

Take it from me, wengine feki tu.... today @ Serena Hotel | From 20:00 to 21:00 #NumberOne…

Take it from me, wengine feki tu.... today @ Serena Hotel | From 20:00 to 21:00 #NumberOne…
Copyright © 2014 TipTop Connection and Blogger Templates - John Sambila.