BABU TALE AELEZEA CHANZO CHA KIFO CHA KAKA YAKE ABDU BONGE



Abdu Bonge aliekuwa Meneja aliekuwa akiongoza Kundi la Muziki la Tiptop Connection akisaidia na Mdogo wake Babu Tale alifariki Dunia jana Jioni, Taarifa za Mwanzo hazikuweza kueleza kuhusu chanzo cha kifo chake lakini leo Mdogo wake Babu Tale ameelezea Jinsi ambavyo kaka yake alipoteza Maisha.
‘Kuna mshkaji wetu mmoja alikua anagombana na mke wake jirani yetu, wakamfata hapa Abdul aende… mara ya kwanza na ya pili akakataa, mara ya tatu akasema ngoja aende’
‘Alivyoenda ukapita ukimya kidogo, baadae kuna mtu akaja kumuita kaka yetu mkubwa mwingine na kumwambia nenda kamsaidie kaka yako mkubwa amedondoka, kaka yangu baadae akanipigia simu akasema Bonge kama amezimia lakini sidhani kama atapona sababu wakati wa kuamulia ugomvi alianguka baada ya kusukumwa nafikiria aliangukia kichogo, kumpeleka Hospitali Manzese wakasema ameshafariki‘ alisema  Babu Tale.

PICHA; MSIBANI TIPTOP CONNECTION


Abdu Bonge alifariki jana Nyumbani majira ya Jioni alipokuwa akiamulia ogovi wa watu wake wa karibu ndipo alianguka vibaya kwenye sakafu na kupoteza Maisha, Mwili bado uko hosptal kwa Uchunguzi zaidi na taratibu zikikamilika kesho mwili utasafirishwa kuelekea Morogoro Mbuyuni Kilometa takribani 100 kutokea Morogoro Mjini ambako ni Nyumbani kwa Marehemu. kwa sasa msiba upo Magomeni Njiapanda ya Kagera maskani ya Tiptop Connection.

PICHA ZAIDI INGIA >>HARAKATI ZA BONGO
 MB Doggy Msanii kutoka TipTop Connection akizungumza jambo na Rafiki waliotembelea Msibani hapo.
 Mkubwa Fella akipitisha Daftari la michango kwa Ndugu na Jamaa waliofika Msibani.
 Mdogo wa Marehemu Mjomba Iddi mwenye Fulana Nyekundu akizungumza jambo na Rafiki Msibani hapo.
 Mdogo wa Marehemu Kwembe Taletale a.k.a DJ K Man mwenye Fulana Nyeusi akizungumza jambo na Ndugu na Jamaa Msibani hapo.
 Tunda man Akilia kwa Uchungu kabisa akiwa na Babu Tale Msibani Magomeni Njiapanda ya Kagera Maskani ya Tiptop Connection.

NEW VIDEO: CHEGE NA TEMBA FEAT MAROMBOSO ~ WAUWE

NEW MUSIC: SHAA ~ SUBIRA

MEW MUSIC: MADEE ~ NI SHEEDA

Rais kutoka Manzese ameachia Mpini wake mpya leo ambao unaitwa Ni Sheedah, Track hii imefanyika kwa Marco Chali pale MJ Rec, Madee amesema ngoma hii haina ujumbe wowote ila ni Ngoma ya Kupaty tu. isikilize hapa kisha kama unalolote weka maoniyako kwa hapo chini....

NEW MUSIC: YAMOTO BAND ~ NITAJUTA

Vijana wenye Maskani yao TMK ambao walifanya poa sana wimbo wao wa Yamoto na kupata jina la Yamoto Band, Aslay, Becka, Bella na Maromboso kutoka Mkubwa na wanawe wameachia wimbo wao wapili ambao unaitwa NITAJUTA. Wimbo umefanyika katika studio zao chini ya Producer Shirko, Tumia dakika zako 4 kuusikiliza na kama umeuelewa unaweza kuacha Comment yako hapo chini.

NEW VIDEO: YAMOTO BAND ~ NITAJUTA

Yamoto Band kutoka Mkubwa na wanawe, Wameachia Wimbo wao wa pili ambao unaitwa NITAJUTA, Wimbo huu umetengenezwa katika Studio zao chini ya Producer Shirko. Yamoto Band inaundwa na Vijana wanne wenye sauti za hatari na Uwezo wa kuimba,  Becka, Enock Bella, Maromboso pamoja na Aslay ambe ni kiongozi wa kundi.
Copyright © 2014 TipTop Connection and Blogger Templates - John Sambila.